Trump asaini kujengwa ukuta kati ya nchi yake na Mexico

Jan 26

Rais wa Marekani Donald Trump amesaini amri ya Rais inayotaka kujengwa kwa ukuta kati ya nchi yake na Mexico, ikiwa ni ahadi yake kubwa aliyoitoa wakati wa kampeni za uchaguzi.

Akizungumza na kituo cha televisheni cha ABC amesema kazi ya kujenga ukuta huo itaanza ndani ya mwezi mmoja, na kusisitiza kuwa Mexico watatakiwa kulipia.

Rais Trump amesema Mexico itarejesha gharama, hatua ambayo imepingwa na serikali ya Mexico.

Rais Trump pia amesaini amri nyingine ya Rais ya kuimarisha ulinzi.

Ameripotiwa pia kupitia upya mbinu zinazotumiwa kuwahoji washukiwa wa ugaidi, na pia kufungua tena magereza ya siri yanayoendeshwa na Shirika la Kijasusi la nchi hiyo CIA nje ya Marekani.