TB JOSHUA AWASILI JIJINI DAR ES SALAAM

Nov 30

Wakati Rais mteule wa Tanzania, Dokta John Magufuli akitarajiwa kuapishwa Alhamisi , wageni mbalimbali wameanza kuwasili nchini, ambapo leo Mtume TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations nchini Nigeria ametua jijini Dar es Slaam tayari kushuhudia kuapishwa kwa rais huyo wa awamu ya tano. Mara tu baada ya kutua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, TB Joshua alikwenda moja kwa moja Ikulu kumsalimia Rais Jakaya Kikwete na kumpongeza kwa kufanikisha uchaguzi mkuu kwa uhuru na amani. TB Joshua pia amempongeza Rais Kikwete kwa kumpata Dokta Magufuli kuwa mrithi wake na kumtakia Rais huyo wa Tanzania Baraka na Fanaka Tele katika awamu hii mpya ya uongozi wa nchi.