RUFAA YA PISTORIUS YAANZA KUSIKILIZWA:

Nov 03

Waendesha mashtaka wa Afrika Kusini, wameanza kusikiliza rufani kuhusiana na kesi ya Mwanariadha mwenye ulemavu wa miguu Oscar Pistorius kwamba aingizwe kwenye hatia ya mauaji ya mpenzi wake Reeva Steenkamp.

Mwanariadha huyo alitolewa gerezani mwezi uliopita baada ya kutumikia kifungo chake kwa muda wa mwaka mmoja kati ya miaka mitano aliyohukumiwa hapo awali.

Pistorius alimuua  mpenzi wake huyo wakati akiwa bafuni mwaka 2013, japo yeye mwenyewe amekuwa akisisitiza kuwa alidhani ni mvamizi.

Oscar Pistorius anaweza kurudishwa jela kama rufani hii itabadilisha maamuzi ya awali, japo kwa sasa anatumikia kifungo cha nyumbani na haruhusiwi kwenda kusikiliza kesi hiyo inayoendeshwa kwenye mahakama kuu ya rufaa huko mjini Bloemfontein