RAIS WA MISRI APINGA ( IS) KUHUSIKA NA AJALI YA NDEGE YA URUSI

Nov 03

Rais wa Misri Abdul Fattah al-Sisi ameyaelezea madai ya wanamgambo wa kundi la IS kuhusika na kuanguka kwa ndege ya Urusi Jumamosi ya wiki iliyopita katika eneo la Sinai, huku akizitaja taarifa hizo kuwa ni ‘propaganda’.

Kwa mujib wa shirika la utangazaji la BBC, rais Fattah al Sisi amesema kuwa ilikuwa mapema mno kutaja chanzo cha ajali hiyo iliyoua takribani watu 224.

Rais huyo pia ameonya kurukia hitimisho juu ya chanzo cha tukio hilo na kutoa wito kwa wote wenye mapenzi juu ya tukio hilo kushiriki katika uchunguzi.

“Panapokuwepo na propaganda kwamba ndege ilianguka kwasababu ya Isis, hii ni ni moja ya njia za ya kuharibu uimara na usalama wa Misri na hata taswira yake. Niamini mimi, hali katika eneo la Sinai haswa katika maeneo yaliyowekewa mipaka, lipo chini ya uangalizi wetu” alisema rais Sisi.