RAIS MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA WIZARA YA FEDHA

Nov 30

Katika siku yake ya kwanza ofisini akiwa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dokta John Magufuli ameanza utekelezaji wa majukumu yake kwa mtindo usiozoeleka pale alipoamua kutembea kwa mguu kutoka Ikulu kwenda wizara ya Fedha na kukagua utendaji kazi wa wafanyakazi kutoka ofisi moja baada ya nyingine, na kubaini baadhi ya watendaji kutokuwepo ofisini muda wa kazi. Ziara hiyo imefanyika muda mfupi baada ya kumaliza zoezi la kumuapisha mwanasheria mkuu wa serikali aliyemteua siku ya kuapishwa kwake, Bwana George Mcheche Masaju.