MAALIM SEIF AMEWATAKA WANANCHI KUWA WATULIVU

Nov 01

Maalim Seif amewataka wafuasi wake na wazanzibari kwa ujumla kuwa watulivu wakati mazungumzo na Chama hicho pamoja na taasisi mbalimbali za kimataifa ikiwemo Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na msajili wa vyama vya siasa jaji Francis Mutungi. Kiongozi huyo amesema kuwa mazungumzo hayo yanakwenda vema na anatarajia kuwa yatazaa matunda. Amesema pia kuwa amekutana na baadhi ya viongozi na watendaji waandamizi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC ambao amewaomba kumuunga mkono dhidi ya uamuzi na tamko la Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha la kufuta matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25. Kwa mujibu wa Maalim Seif CUF haikubaliani na uamuzi wa kurudiwa kwa uchaguzi huo. Hata hivyo, Maalim Seif amekana kuwepo kwa mazungumzo mengine yoyote na viongozi wa kisiasa hapa nchini na kudai kuwa kuna baadhi ya viongozi wa chama Tawala CCM ambao wamekuwa wakifanya jitihada za kufanya naye mazunguzo bila mafanikio.