AJALI NYINGINE YA NDEGE YATOKEA SUDANI KUSINI:

Nov 04

Ndege ya mizigo imeanguka nchini Sudani Kusini wakati ikiwa inapaa karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa uliopo Juba, mji mkuu wa nchi hiyo huku takribani watu 25 wakihofiwa kupoteza maisha. Baadhi ya taarifa zinasema kuwa idadi ya vifo yaweza kufika watu 40. Bado haijafahamika vema waathirika wangapi walikuwepo kwenye ndege hiyo na wangapi walikuwa uwanjani. Radio Miraya iliyopo mjini Juba inasema kwamba ndege hiyo ilikuwa inaelekea eneo la Upper Nile na kuanguka ikiwa katika umbali wa nusu maili kutoka katika njia ya kurukia na kutulia ndege. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters linaaarifu kuwa Msemaji wa rais wa Sudani Kusini Ateny Wek Ateny, amesema kuwa kulikuwa na takribani wahanga wawili wa ajali hiyo, mmoja ni mfanyakazi wa ndege hiyo na mwingine ni mtoto.