WAZIRI MKUU WA ROMANIA ATANGAZA KUJIUZURU:

Nov 04

Waziri mkuu wa Romania Victor Ponta ametangaza kujiuzulu wadhifa wake ikiwa ni siku moja baada ya takribani watu 20000, kuingia mitaani kupinga tukio la moto liliotokea kwenye klabu ya usiku na kusababisha vifo vya watu 32. Maandamano hayo yamefanyika kwa lengo la kumtaka Ponta kujiuzulu wakiilalamikia Serikali juu ya swala la rushwa na usimamizi mbovu wa usalama. Bwana Ponta tayari anakabiliwa na mashtaka kuhusiana na rushwa na anakuwa Waziri mkuu wa kwanza wa nchi hiyo kutuhumiwa kujihusisha na rushwa katika kipindi cha kiangazi akikabiliwa na madai ya udanganyifu, ukwepaji kodi na matumizi ya fedha chafu kwa miaka kadhaa.